Lugha ya Kigogo inazungumzwa na watu zaidi ya milioni moja hasa katika mkoa wa Dodoma. Ingawa kuna maandiko kadhaa katika lugha ya Kigogo, kamusi hii ni ya kwanza kuandaliwa kwa lugha hii, ukiondoa orodha ya Mwalimu William Mlagulwa yenye maneno 4821. Maandiko mengi yaliyopo yanahusiana na dini ya Kikristu. Jitihada hizo za maandiko ya Biblia zimetoa mchango mkubwa katika kusanifisha lugha hii. Hivyo kamusi hii imefuata kwa karibu taratibu zilizokubalika katika maandiko hayo.








